Sonko akamatwa, mkutano wake ukitibuliwa

0

Gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko ameshikwa na kisha kuachiliwa baada ya Polisi kutumia vitoa machozi kutibua mkutano wake na wawakilishi wadi wanaomuunga mkono katika eneo la Riverside, Nairobi.

Hata hivyo haijabainika mara moja ajenda ya mkutano huo ilikuwa ni nini ila inaarifiwa kuwa Polisi waliutubua kwa sababu ya kutekeleza masharti ya kuzuia msambao wa virusi vya corona.

Ni mkutano unaojiri wakati ambapo Sonko anakabiliwa na tishio la kubanduliwa mamlakani.

Wana Nairobi wana hadi Jumatano wiki hii kuwasilisha maoni yao kuhusu hoja hiyo.

Jumla ya wawakilishi wadi 86 kati ya 122 wametia sahihi zao kwenye mswada huo wa kumuondoa.

Mswada huo uliwasilishwa bungeni na kiongozi wa walio wachache Michael Ogada.

Ma MCAs wanaomuunga mkono Sonko wametaja kuwa njama ya kumbandua imesababishwa na hatua yake kukataa kutia saini na kuidhinisha bajeti inayogharimu Sh37.5b ya mwaka 2020-2021.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here