Someni BBI na muelewe, Uhuru awaambia Wakenya

0

Huku mjadala kuhusu ripoti ya BBI ikiendelea kuibua hisia mseto kote nchini, wakenya wametakiwa kuisoma kwa umakini ripoti hiyo na kuzingatia mapendekezo yake.

Rais Uhuru Kenyatta ametumia hotuba yake ya saba kwa taifa kuwasihi Wakenya kuisoma ripoti hiyo na kuilewa ili kuwezesha taifa hili kutatua changamoto ambazo zimekuwa zikilikumba kwa muda mrefu.

Miongoni mwa changamoto ambazo rais ametaja ni pamoja na siasa zilizojikita kwa ukabila.

Rais Kenyatta ambaye amesema mataifa jirani yanahitaji handisheki vile vile amewaonya viongozi dhidi ya kuwatumia vijana kujitafutia umaarufu wa kisiasa.

Naibu rais William Ruto, kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga, mwenzake wa Wiper Kalonzo Musyoka na Musalia Mudavadi wa ANC walikuwepo wakati wa hotuba hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here