SOKO KWA MAZAO YA KENYA, UPANUZI WA SGR – MATUNDA YA SAFARI YA RUTO UCHINA.

0
Rais wa Kenya Wiliam Ruto (Kulia) na Xi Jinping wa China wakutana kabla ya Mkutano wa tisa wa Wakuu wa Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) utakaofanyika Beijing, China Septemba 3, 2024. | PICHA: PCS

Uchina imekubalia mazao kutoka hKenya kuuzwa katika masoko yake kufuatia makubaliano kati ya rais William Ruto na rais wa uchina Xi Jinping.

Rais Ruto anaehudhuria kikao cha 9 cha ushirikiano baina kenya na uchina amesema kuwa makubaliano hayo yameafikiwa katika kikao cha faragha baina yake na Jinping.

Maraias hao aidha wamekubaliana kuhusu ufadhili wa miundo msingi ikiwemo upanuzi wa reli ya kisasa ya SGR na kukamilishwa kwa ujenzi wa barabara ya Rironi- Mau Summit.

“Nilifanya mazungumzo na Rais Xi Jinping kwenye Ukumbi Mkuu wa Watu huko Beijing, Uchina, kabla ya Mkutano wa Wakuu wa Jukwaa la Ushirikiano wa China Afrika (FOCAC). Wakati wa mkutano huo, Rais Xi alikubali kuruhusu mazao ya kilimo ya Kenya kufikia soko la Uchina,” Ruto amesema kwenye Ukurasa wake wa X.

Ofisi ya rais haijatoa maelezo zaidi kuhusu mazao ya kilimo yatakayoruhusiwa kuingia uchina au masharti ya mkataba huo wakati wa kikao na vyombo vya habari.

Ruto amesema upanuzi wa reli ya Standard Gauge Railway (SGR) kutpka Mombasa hadi mjini Naivasha pia umejadiliwa wakati wa mkutano wake na Jinping.

Rais wa Kenya Wiliam Ruto (Kulia) na Xi Jinping wa China wakutana kabla ya Mkutano wa tisa wa Wakuu wa Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) utakaofanyika Beijing, China Septemba 3, 2024. | PICHA: PCS
Rais wa Kenya Wiliam Ruto (Kulia) na Xi Jinping wa China wakutana kabla ya Mkutano wa tisa wa Wakuu wa Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) utakaofanyika Beijing, China Septemba 3, 2024. | PICHA: PCS
“Tulijadili pia miradi ya miundombinu ya kikanda kama vile upanuzi wa SGR, na njia ya uchukuzi ya Rironi-Mau Summit-Malaba,” Rais ameandika kwenye X.

SGR iliyogharimu dola bilioni 3.6 ni miongoni mwa miradi ya miundombinu ambayo China imefadhili nchini Kenya, pamoja na Barabara ya Nairobi Expressway katika mji mkuu.

Rais Ruto yumo nchini Uchini kuhudhuria Mkutano wa FOCAC unaowaleta pamoja Wakuu wa Nchi za Afrika, viongozi wa China na Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC) ili kujadili na kuimarisha uhusiano kati ya China na Afrika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here