Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi sasa anasema hataomba msamaha kufuatia matamshi yake kuhusu familia ya rais Uhuru Kenyatta.
Akiwahutubia waandishi wa habari nyumbani kwake, Sudi amesema matamshi yake hayakuwa na matusi na badala yake kutaka aombwe msamaha na wale wanaomkosoa.
Mbunge huyo vile vile amesema hajatumwa na naibu rais William Ruto kuzungumza kwa niaba yake na badala yake kusema matamshi yake yamechochewa na msimamo wake binafsi.
Mbunge wa Maragua Mary Waithira pamoja na aliyekuwa kiongozi wa wanawake Jane Kiano wamekuwa viongozi wa hivi punde kukashifu matamshi hayo na kumtaka Sudi na mwenzake wa Emurua Dikirr Johana Ng’eno kuomba msamaha.
Yakijiri hayo
Baadhi ya vijana katika kaunti ya Nakuru wameandamana kuonyesha kuchukizwa kwa matamshi ya wabunge hao wawili huku wakiwataka wawili hao kuwa na heshima hasa kwa akina mama.