Sikusema Ruto ajiuzulu – Matiang’i

0

Waziri wa Usalama wa ndani Fred Matiang’i amekanusha madai kuwa alimtaka naibu Rais William Ruto kujiuzulu kwa kukashifu kukamatwa kwa maseneta watatu.

Katika taarifa, Matiang’i anasema hakutoa matamshi kama hayo alipokuwa anahojiwa na kamati ya senti kuhusu usalama na kutaja ripoti hizo katika baadhi ya vyombo vya habari kuwa za kupotosha.

Matiang’i anasema taarifa kama hizo zina uwezo wa kuzua mgawanyiko serikalini na kusema amewaagiza mawakili wake kushtaki wanahabari waliochapisha uvumi huo.

Matiangi anadaiwa kutoa matamshi hayo alipokuwa anahojiwa na kamati hiyo chini ya uenyekiti wa seneta wa Garissa Yusuf Haji kuhusiana na kukamatwa kwa maseneta wattau siku ya Jumatatu.

Matiangi alisema kukamatwa kwa maseneta hao Cleophas Malala wa Kakamega, Steve Lelegwe wa Samburu na Christopher Langat wa Bomet hakuna uhusiana wowote na mswada tata wa ugavi wa mapato.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here