Siasa za BBI zatawawala sherehe za Mashujaa

0

Siasa za BBI zimetawala maadhimisho ya mwaka huu ya siku kuu ya Mashujaa zilizoandaliwa katika uwanja wa Gusii kaunti ya Kisii.

Rais Uhuru Kenyatta aliyeoongoza sherehe hizo za kumi na moja ametumia sherehe hizo kupigia debe marekebisho ya kikatiba kupitia BBI.

Rais Kenyatta ambaye hakusitasita katika maneno yake amewajibu wanaopinga BBI wakiongozwa na naibu wake William Ruto wanaodai kuwa maazimio ni kubuni nafasi zaidi kwa viongozi.

Badala yake rais amesema lengo kuu la marekebisho hayo ya kikatiba ni kuzika katika katika kaburi la sahau uhasama wa mara kwa kila baada ya uchaguzi.

Kwa upande wake, naibu rais William Ruto ametoa wito kwa kila mkenya kuhusihwa kwenye mchakato huo mzima wa kuifanyia katiba marekebisho.

 Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga aliyezungumza kabla ya Dr Ruto alisema kampeini za kupigia debe ripoti hiyo ya BBI zitarejea baada ya kusitishwa na janga la corona ila akasema hili ni kwa kuzingatia mwongozo utakaotolewa na rais.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here