Shule kufunguliwa Jumatatu ijayo atangaza Magoha

0

Shule zitafunguliwa kwa wanafunzi wa darasa la nne, darasa la nane na kidato cha nne kuanzia Jumatatu ijayo huku mitihani ya kitaifa ya KCPE na KCSE ikifanyika mwaka ujao.

Waziri wa elimu Profesa George Magoha ametangaza kuwa mitihani ya KCPE itaanza Machi 22 na kukamilika Machi 24 mwaka 2021.

Mitihani ya kitaifa ya kidato cha nne KCSE inatazamiwa kuandaliwa kati ya Machi 25 na Aprili 16 mwaka ujao.

Wanafunzi hao watasoma kwa majuma 11 kabla ya kufunga shule kwa likizo Disemba 23 na kisha kufungua tena tarehe 01-01-2021.

Muhula wa tatu kwa wanafunzi hao utaanza 04-01-2021 na kuendelea kwa majuma 11 hadi 19-03-2021.

Waziri Magoha aidha ametangaza kuwa tayari serikali imegharamia ada zote za mitihani ya KCPE na KCSE na hivyo kuwashauri wazazi kuwaandaa wanao tayari kurejea shuleni kuanzia Jumatatu.

Haya yanajiri siku moja baada ya wanafunzi wa mwaka wa mwisho katika vyuo vikuu na vyuo anuai kurejea shuleni baada ya masomo kusitishwa kutokana na janga la kimataifa la corona.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here