Serikali haitafunga shule licha ya wazazi kuingiwa na hofu kufuatia kuongezeka kwa msambao wa visa vya corona amesema waziri wa elimu Profesa George Magoha.
Badala yake waziri Magoha amewataka wazazi na walimu kuendelea kuwaandaa watahiniwa kukalia mitihani yao ya kitaifa mwaka ujao huku akisisitiza kuwa kalenda ya mitihani ya KCPE na KCSE haitabadilishwa.
Na huku baadhi ya shule zikifungwa baada ya kuripoti visa vya COVID19, waziri Magoha amesema wadau watakutana hivi karibuni kujadiliana kuhusu ni lini shule zitafunguliwa rasmi kwa kuzingatia hali ya msambao wa virusi hivyo.
Profesa Magoha amesema haya alipokagua mradi wa serikali kutoa madawati katika shule ya msingi ya Uhuru Gardens iliyoko Lang’ata jijini Nairobi.