Shughuli za michezo nchini kurejea karibuni

0

Wana michezo nchini wana sababu ya kutabasamu baada ya serikali kuzindua mwongozo utakaotumika kurejesha shughuli za spoti nchini.

Waziri wa Michezo Balozi Amina Mohammed amewapa washikadau muda wa siku saba  kutoa maoni  yao kuhusu mapendekezo yaliyopo kwenye mwogozo huo uliotayarishwa na kamati maalum aliyoteua.

Miongoni mwa mapendekezo kwenye mwongozo huo yaliyosomwa na katibu wa michezo Joe Okudo ni kuzingatiwa kwa masharti yaliyotolewa na wizara ya afya afya ikiwemo kuvalia barakoa na kukaa umbali wa mita moja unusu.

Serikali ilisitisha shughuli za michezo kama njia moja ya kukabili maambukizi ya virusi  vya corona nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here