Serikali yatoa pesa za elimu ya bwerere

0

Serikali imetoa Sh14.5b kufadhili masomo ya bure katika shule za upili huku shule zikitazamiwa kufunguliwa Jumatatu ijayo Octoba 12.

Katibu mkuu katika wizara ya elimu Belio Kipsang anasema pesa hizo zitafika shuleni kufikia Jumatatu wakati wanafunzi wa darasa la nne, darasa la nane na kidato cha nne wataripoti shuleni.

Wakuu wa shule wametakiwa kuhakikisha kuwa masharti ya usalama kuzuia msambao wa virusi vya corona yanafuatwa huku mitihani ya kitaifa ya darasa la nane KCPE na kidato cha nne KCSE ikitazamiwa kufanywa mwaka ujao.

KCPE itaanza Machi 22, 2021 na kukamilika Machi 24, 2021 huku mitihani ya KCSE ikikaliwa kuanzia Machi 25 hadi Aprili 16.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here