Serikali yatetea Huduma Namba

0

Serikali imekana madai yaliyotolewa na wendani wa naibu rais William Ruto kwamba inapanga kutumia raia wa kigeni kusimamia usajili wa Huduma Namba kwa malengo ya kumuibia Ruto kura.

Waziri wa usalama wa ndani Dkt. Fred Matiang’i badala yake amesema Huduma Namba ni mfumo wa serikali ya Kenya na unasimamiwa na Wakenya na sio wageni kama ilivyodaiwa na mbunge wa Kikuyu Kimani Ichungwa na Aisha Jumwa wa Malindi.

Waziri Matiang’i ameongeza kwamba utoaji wa kadi za Huduma Namba kufuatia kukamilika kwa zoezi la kwanza unatazamiwa kuanza kabla ya mwisho wa mwaka huu

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here