Serikali imelaani vikali uozo wa wizi wa watoto wachanga unaoendelezwa nchini kufuatia makala ya ufichuzi yaliyopeperushwa na shirika la habari la BBC.
Waziri wa Leba na maswala ya kijamii Simon Chelugui amesema kumebuniwa kundi la pamoja kuanzisha uchunguzi kuhusiana na sakata hiyo kwa malengo ya kuwaadhibu wahusika.
INSERT: CHELUGUI ON SAKATA YA WATOTO
Katika makala hayo, ilifichuliwa kwamba watoto wanauzwa kwa kati ya Sh70,000 hadi Sh300,000 baada ya kuibwa.
Biashara hiyo haramu imekuwa ikiendelezwa katika kliniki haramu jijini Nairobi sawa na baadhi ya hospitali za umma.









