Watoto kutoka jamii maskini katika Kaunti ya Nairobi wanatazamiwa kufaidika na chakula cha mchana bila malipo, kwa hisani ya serikali ya kitaifa na ile ya kaunti.
Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu amefichuwa kuwa chakula kitatolewa kwa wanafunzi wachanga katika shule za msingi za umma chini ya mpango wa ‘Lishe Shuleni’.
Machogu ambaye alikuwa akizungumza baada ya mkutano wa mashauriano na Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja na Mbunge wa Dagoretti Kusini John Kiarie amebainisha kuwa mpango huo utawezesha watoto kuendelea na masomo yao bila kchangamoto ya lishe.
“Mpango huu utaboresha motisha ya wanafunzi hasa wale wanaotoka katika vitongoji duni na makazi yasiyo rasmi jijini Nairobi,” alisema waziri Machogu .
Kupitia akaunti yake ya twitta gavana sakaja amesema mpango utaanza kutekelezwa mwanzoni mwa muhula wa tatu.
Gavana sakaja ameongeza kuwa serikali yake inanuia kuendeleza ushirikiano na wizara ya elimu katika sekta mbalimabli.
“Pia tilizungumza maeneo mengine ya ushirikiano ikiwa ni pamoja na TIVETs , kutoa ardhi kwa mashule, upanuzi wa miundombinu ya Elimu ya Sekondari na uboreshaji wa vifaa kwa ajili ya watoto wetu.’ Alisema Sakaja.