SENETI YADINDA KUIDHINISHA KAMATI SPESHELI KUSIKILIZA HOJA DHIDI YA GACHAGUA

0
KINGI NA GACHAGUA
KINGI NA GACHAGUA

Hoja ya kumtimua afisini Naibu wa Rais Rigathi Gachagua itasikilizwa na kuamuliwa na maseneta wote.

Hii ni baada ya pendekezo la kubuniwa kwa kamati spesheli kuchuguza madai hayo iliyowasilishwa na Kiongozi wa Wengi Seneta Allan Cheruiyot kufeli.

Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna aliyepaswa kuunga mkono pendekezo hilo amekosa kufanya hivyo na kupisha tangazo la spika kuwa maseneta wote watachunguza mswaada huo.

“ Seria zinasema kuwa iwapo pndekezo hili litakosa kuungwa mkono basi linatupiliwa mbali. Hivyo naagiza swala hili lisikilizwe na maseneta wote,” ameagiza Spika Kingi Jeffa.

Vikao vya kujadili na kuchunguza mswaada huo utakuwa wa hadhara.

Gachagua ataitaji uungwaji mkono wa thuluthi moja ya maseeta amba oni maseneta 23 kumuunga mkono ili kuzima jaribio la kumtimua.

Hoja Maalum ilitaja mashtaka 11 dhidi ya Naibu Rais, yakiwemo ukiukaji mkubwa wa Katiba, kuhujumu Rais na Baraza la Mawaziri, kudhoofisha Ugatuzi, na kuathiri uhuru wa mahakama kwa kumshambulia jaji hadharani.

Mashtaka mengine ni pamoja na kutoa taarifa za uchochezi, kutenda uhalifu wa kiuchumi, kueneza matamshi ya uwongo, yenye nia mbaya, yenye migawanyiko na uchochezi, kutotii Rais hadharani, na kuwaonea maafisa wa Serikali na wa umma.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here