Seneta wa Machakos Boniface Kabaka afariki

0

Seneta wa kaunti ya Machakos Boniface Mutinda Kabaka ameaga dunia.

Kabaka amefariki akiendelea kupokea matibabu katika hospitali ya Nairobi ambapo amekuwa kwa wiki moja katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).

Seneta huyo alikimbizwa hospitalini baada ya kuanguka na kuzirai katika eneo la Kilimani Nairobi.

Polisi wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na kilichomkuta seneta huyo huku mwanamke aliyekuwa naye Esther Nthenya akikamatwa na kisha kuachiliwa bila kufunguliwa mashtaka.

Rais Uhuru Kenyatta amewaongoza viongozi wengine kumuomboleza seneta huyo akimtaja kama kiongozi aliyejitolea kuwahudumia wananchi.

Katika risala zake, rais ameifariji familia ya marehemu na kumuomba Mungu awape Mungu wakati huu wa msiba.

Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka amemuomboleza marehemu akitoa wito kwa umma kuipa familia muda wa kuomboleza.

INSERT: KALONZO ON KABAKA

 Kabaka amewaacha wajane wawili Jennifer na Katanu pamoja na watoto.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here