Seneta wa kuteuliwa Sylvia Kasanga ndiye mwenyekiti mpya wa kamati ya bunge inayoangazia swala la COVID19 baada ya kujiuzulu kwa seneta wa Nairobi Johnson Sakaja.
Kasanga amekuwa akihudumu kama naibu mwenyekiti wa kamati hiyo iliyotwikwa jukumu la kumulika namna serikali inavyoshughulikia swala la corona nchini.
Sakaja alijiuzulu kama mwenyekiti wa kamati hiyo baada yake kukamawa na kushtakiwa kwa kukaidi masharti ya kafyuu.









