Sakata ya KEMSA: DPP ateua kundi la waendesha mashtaka

0

Mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma DPP Noordin Hajji ameteua kundi la waendesha wa mashtaka kuchunguza madai ya ufujaji wa Sh7.8b za  kukabiliana na janga la COVID19 katika shirika la kununua dawa na kusambaza vifaa vya matibabu KEMSA.

Katika taarifa, Hajj amesema ameteua kundi hilo la waendesha mashtaka baada ya kupokea faili ya uchunguzi kutoka kwa tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC.

Kundi hilo linatazamiwa kukamilisha uchunguzi wake kwa muda wa siku kumi na nne na kisha kurejesha matokeo kwa Hajji.

Hajji amesema atatoa mwelekeo utakaofuata baada ya kupokea matokeo ya uchunguzi huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here