Ruto: Rasilimali zaidi zitumwe mashinani

0

Kuna haja ya maeneo tengwa nchini kupewa rasilimali zaidi ili kuyawezesha kuafikia ajenda ya maendeleo.

Ndio kauli yake naibu rais William Ruto ambaye anasema afya, elimu na miundo mbinu inapaswa kupewa kipau mbele katika maeneo hayo ili kuhakikisha kuwa wananchi wamepata maendeleo kama sehemu zingine.

Ruto amesema haya alipokutana na viongozi wa kisiasa na wale wa kidini wa kaunti ya Narok katika afisi zake zilizoko Karen, Nairobi.

Kauli za naibu rais zinawadia wakati ambapo mjadala mkali unaendelea nchini kuhusu mswada wa ugavi wa mapato ambao umesababisha migawanyiko miongoni mwa viongozi.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here