Ruto aweka wazi mapungufu kwenye ripoti ya BBI

0

Naibu rais William Ruto ameibua mjadala mkali kuhusu ripoti ya BBI katika ukumbi wa Bomas licha yake kuzomewa wakati wa hotuba yake.

Mwanzo, Ruto ametaka maelezo kuhusu ni vipi kuwepo kwa afisi ya waziri mkuu, manaibu wake wawili na afisi ya kiongozi wa upinzani itashughulikia suala la mshindi katika uchaguzi wa urais kuchukua kila kitu huku aliyeshindwa akiambulia patupu.

Niabu rais vile vile ametofautiana na wazo la kuwaruhusu wanasiasa kuwachagua baadhi ya makamishna wa tume ya uchaguzi na mipaka IEBC akisema itatoa mwanya wa kukosekana kwa uwazi na usawa katika mchakato mzima wa uchaguzi.

Mwisho wa siku, naibu Rais ambaye ameonekana kuipinga ripoti hiyo, anasema wakenya wanafaa kuelezea kwa kina vile mapendekezo yake yataleta suluhu la masuala mbalimbali kabla ya kushiriki kura ya maamuzi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here