Ruto awaonya watumishi wa umma

0

Naibu rais William Ruto amewaonya watumishi wa umma dhidi ya kukubali kutumiwa kutekeleza ajenda za kisiasa.

Akizungumza katika afisi zake Karen alipotoa msaada kwa makundi ya vijana kutoka Kibra na Langata, Ruto amewataka watumishi wa umma haswaa Polisi kuzingatia maadili mema ya utendakazi wanapowajibikia majukumu yao.

Naibu rais vile vile amewakanya wanasiasa dhidi ya kuwatumia Polisi kuwatishia wapinzani wao akisema hilo halitakubalika chini ya katiba.

Matamshi ya Ruto yanawadia siku chache baada ya kukamatwa kwa maseneta watatu kufuatia tofauti zilizoibuka kuhusu mswada tata wa ugavi wa mapato.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here