Ruto awakemea walioiba pesa za corona

0

Naibu rais William Ruto anadai kuwa watu fulani waliokuwa wamefilisika kwa sasa wamekuwa mabilionea baada ya kuiba pesa za corona na kumsingizia yeye.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, naibu rais amewasuta watu hao ambao hakuwataja kwa kuwaibia wagonjwa hata wakati wa janga.

Amesema mwisho wao unakaribia na hawatakuwa na mahali pa kujificha na kwamba hakutakuwa na mtu wa kisingizia wizi huo.

Matamshi ya Ruto yanawadia wakati ambapo asasi za husika zinachunguza madai ya wizi wa pesa zilizotengwa kwa minajili ya kupambana na janga la corona.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here