Ruto ataka kura ya maamuzi iandaliwe na uchaguzi 2022

0

Naibu rais William Ruto na wendani wake sasa wanataka kura ya maamuzi kufanyia katiba marekebisho kuandaliwa sambamba na uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.

Ruto akizungumza baada ya kufanya mkutano wa mashauriano na wendani wake wakiwemo wabunge na magavana Karen, Nairobi wamesema itakuwa ghali mno kuandaa kura ya maamuzi mwaka ujao na kisha kushiriki uchaguzi mkuu mwaka unaofuatia.

Viongozi hao badala yake wanataka pesa zitakazotumiwa kwenye kura ya maamuzi kubadilisha katiba kutumika katika kupambana na janga la COVID19.

Wanasiasa hao vile vile wametoa wito wa kufanyika kwa mazungumzo zaidi kuhusu mswada -wa BBI ili kuafikia maelewano ikiwemo kuongeza idadi ya wabunge pamoja na swala la kubuniwa tume ya kupokea malalamishi kuhusu utendakazi wa idara ya mahakama.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here