Ruto akutana na muwaniaji huru Msambweni

0

Naibu rais William Ruto amekutana na muwaniaji huru wa kiti cha ubunge cha Msambweni Feisal Abdallah Bader siku moja baada ya chama cha Jubilee kutangaza kuwa hakitakuwa na muwaniaji katika uchaguzi huo.

Ruto amekutana na muwaniaji huyo katika afisi zake Karen pamoja na wabunge kutoka Pwani akiwemo Athman Shariff (Lamu Mashariki), Mohamed Ali (Nyali), Owen Baya (Kilifi Kusini), Khatib Mwashetani (Lunga Lunga) na Aisha Jumwa wa Malindi.

Hata hivyo haijabanika mara moja iwapo naibu rais atamuunga mkono muwaniaji huyo kwenye uchaguzi utakaondaliwa Disemba 15.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here