Ruto ahepa uzinduzi wa ripoti ya BBI, aenda kwa matanga

0

Naibu rais William Ruto amekwepa kuhudhuria hafla ya kupokezwa ripoti ya BBI kwa rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa chama cha ODM  Raila Odinga.

Badala yake Ruto amehudhuria mazishi ya MCA wa Huruma Peter Chomba katika eneo la Turbo kaunti ya Uasin Gishu aliyefariki wiki moja iliyopita kutokana kile familia yake imetaja kama matatizo yanayoambatana na ugonjwa corona.

Naibu rais amekosa kuhudhuria hafla hiyo siku moja baada ya kutaka mjadala mzima wa kufanyia katiba marekebisho uwajumuishe watu wote pasipo ubaguzi.

Ruto pamoja na wendani wake vile vile wameapa kupinga ripoti hiyo iwapo itapendekeza kuongezwa kwa nafasi za viongozi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here