Rais William Ruto ameifariji familia ya Naibu Gavana wa Meru Isaac M’Ethingia kufuatia kifo cha mamake.
Katika ujumbe wake wa rambirambi, Rais amemuomboleza Mama Joyce …2nd name…kuwa ni mcha Mungu na ameitakia familia yake faraja ya Mungu wakati wakiomboleza kifo chake.
“Rambirambi zetu kwa Naibu Gavana wa Meru Isaac M’Ethingia kwa kifo cha mamake mpendwa, Joyce. Alikuwa mwanamke mwajibikaji, mcha Mungu na ambaye alijitolea kutumikia jamii,” Rais Ruto amesema.
“Mungu aifariji familia na watu wa Meru katika kipindi hiki cha majonzi. Pumzika kwa Amani.” Ameongeza Rais.
Mama Joyce Methingia, aliaga dunia Januari tarehe tano mwaka huu akipokea matibabu katika hospitali ya St. Theresa huko Meru.
Alikuwa na umri wa miaka 93 wakati wa kuaga kwake.
Mama joyce alikuwa mke wa mwenyekiti wa zamani wa baraza la Njuri Ncheke Mzee Paul Methingia.vvv