Rais Uhuru Kenyatta aitisha kikao kujadili kupanda kwa corona Kenya

0

Je, serikali itakaza kamba katika masharti ya kupambana na janga la COVID19?

Ndilo swali Wakenya watatatarajiwa kupata majibu baada ya rais Uhuru Kenyatta kuitisha kikao kinacholenga kutathmini hali ya ugonjwa wa corona nchini kufikia sasa.

Mkutano huo utakoandaliwa Jumatano wiki ijayo ambayo ni Novemba 4 unalenga kuangazia kuongezeka kwa maambukizi ya ugonjwa huo wa corona tangu serikali ilipolegeza masharti ya kupambana na ugonjwa huo.

Kuendelea kupanda kwa maafa yanayotokana na ugonjwa huo vile vile kutajadiliwa kwenye mkutano huo utakaodhuhuriwa na baraza la magavana.

Mabadiliko yanayoambatana na ugonjwa huo sawa na madhara yaliyotokea tangu kulegezwa kwa masharti hayo yatajadiliwa katika kikao hicho muhimu.

Katika ujumbe wake kuelekea kwa kikao hicho, rais Kenyatta amewasihi Wakenya kuendelea kuzingatia masharti salama ya kuzuia msambao wa virusi hivyo ikiwemo kunawa mikono, kuvalia barakoa na kuepuka kukaribiana kwani hili linasalia kuwa jukumu la kila mmoja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here