Rais William ruto amevunja kimya chake kuhusu mgogoro unaoendelea baina ya Idara ya mahakama na afisi ya inspekta jenerali wa polisi.
Akizungumza alipooongoza uzinduzi wa mfumo wa utekelezaji wa mageuzi katika sekta ya polisi Rais Ruto amesema mvutano baina polisi na mahakama italemaza upatikanaji wa haki kwa raia wa kawaida.
“Najua mahakama ni idara huru, polisi pi ni idara huru, lakini tunafanya kazi kwa faida ya mwajiri mmoja ambae ni mkenya wa kawaida. Mivutano hii haifai iwapo tunaazimia kutumikia mkenya wa kawaida” Amesema Rais Ruto.
Kiongozi wa taifa ametaka asasi hizo mbili kuendelea kufanya kazi kwa Pamoja kwa faida ya mkenya wa kawaida.
Hayo yanajiri wakati ambapo Kaimu Inspekta jenerali Gilbetrt Masengeli ameelekea mahakamani kupinga agizo la kuhukumiwa kifungu cha miezi sita gerezani.
Katika Rufaa yake Masengeli amesema kuwa Jaji Lawrence Mugambi alimhukumu pasi na kumpa nafasi ya kujitetea.
Hatua ya kuondolewa kwa walinzi wa Jaji Mugambi siku tatu baada ya kumhukumu Masengeli ilipingwa na jaji mkuu Martha Koome na wahusika wengine walioitaja kama ukiukaji wa haki za jaji huyo na tishio kwa uhuru wa mahakama.