Rais William Ruto amepongeza jukumu la viongozi wa kidini katika jamii, akisema kuwa ni nguzo muhimu katika kudumisha maadili.
Rais ametoa matamshi hayo wakati wa mkutano na viongozi mbalimbali wa kidini kutoka maeneo ya Kiambaa, Kabete na Thika katika Kaunti ya Kiambu.
“Mabadiliko ya nchi yetu yanahitaji juhudi za pamoja kutoka kwa makundi yote ya uongozi, ikiwa ni pamoja na viongozi wa kisiasa na kidini,” Ruto amesema.
Rais ameshukuru viongozi wa kidini kwa mchango wao katika sekta za elimu na afya.
“Tunathamini mchango mkubwa wa viongozi wetu wa kidini katika kudumisha maadili ya jamii yetu,” amesema Rais Ruto.
“Mchango wao katika utoaji wa elimu na utoaji wa huduma za afya ni uthibitisho wa kujitolea kwao kwa ustawi na maendeleo ya taifa letua” aliongeza Rais Ruto.