RAIS RUTO AONDOKA NCHINI KUELEKEA UCHINA

0
Ruto-na-Raila.jpeg
Ruto-na-Raila.jpeg

Rais William Ruto ameondoka humu nchini na kueleka taifa la Uchina kuwakilisha Kenya kwenye kongamano la ushirikiano baina ya Africa na Uchina (Focac

Kongamano hilo linawaleta pamoja Marais wa mataifa ya Africa, viongozi wa taifa la Uchina na tume ya umoja wa Africa (AUC) na linalenga undwaji wa sera za maenedeleo ya kijamii na uchumi.

Katika ziara hiyo, Rais Ruto atakutana na Rais wa Uchina Xi Jingping katika juhudi za kuimarisha mahusiano baina ya Kenya na uchina pamoja na kubaini nyanja tofauti za ushiriakiano

Kiongozi wa taifa pia atakuwa anakutana na viongozi wengine wa mataifa ya Afrika kama vile Senegal na Algeria.

Rais Ruto yupo pamoja na mgombeaji wa wadhifa wa uenyekiti wa AUC Raila Odinga, waziri mwenye mamlaka Musalia Mudavadi na waziri wa hazina ya kitaifa John Mbadi.

Hii inakuwa safari ya pili ya Rais Ruto kuondoka humu nchini tangu kuzuka kwa maaandamano ya kupinga mswada wa fedha mwaka wa 2024/25.

Awali Rais Ruto alizuru taifa la Rwanda kuhudhuria kuapishwa kwa Paul Kagame kama Rais wa taifa hilo mnamo tarehe 11 mwezi Agosti mwaka huu.

Safari ya mwisho ya kiongozi wa taifa kabla ya maandamano ilikuwa tarehe 15 na 16 mwezi Juni katika taifa la Switzerland.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here