Rais Kenyatta kulihutubia taifa leo mchana

0

Rais Uhuru Kenyatta anatazamiwa kulihutubia taifa hii leo mchana kutangaza mikakati mipya ya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

Hotuba hiyo kutoka ikulu ya Rais inatazamiwa kuweka bayana maafikiano ya kikao na washikadau kinachoendelea kutafuta njia za kuzuia kusambaa zaidi kwa virusi vya corona nchini.

Miongoni mwa mikakati mipya inayotazamiwa kutangazwa ni masharti makali ya kuandaliwa kwa mikusanyiko ya watu wengi, muda wa kafyu, masharti ya kudhibiti maeneo ya burudani, miongoni mwa masharti mengine.

Baraza la magavana ambalo limewakilishwa kwenye kikao hicho linataka pia mipaka ya baadhi ya kaunti kufungwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here