Rais Uhuru Kenyatta anatazamiwa kulihutubia taifa hii leo kuhusiana na masharti yaliyowekwa kukabiliana na janga la covid19 nchini.
Amri aliyotoa ya kutotoka nje kati ya saa tatu usiku na saa kumi asubuhi inakamilika hapo kesho, na amiri jeshi mkuu anatazamiwa kutoa mweleko wa iwapo kafyu itaendelea kutekelezwa au itaondolewa.
Baadhi ya wakenya wamekuwa wakiitaka serikali kuondo kafyu ili kuwawezesha kusafiri na kufanya shughuli zingine nyakati za usiku.
Katika hotuba yake kwa taifa tarehe ishirini na saba mwezi uliopita, Rais pia alipiga marufuku uuzaji wa vileo kwenye mikahawa na hoteli na pia kufunga maeneo ya burudani.