Rais Uhuru Kenyatta amewakumbusha watumishi wa umma kuwahudumia wananchi na kujiepusha na mambo yanayohujumu utoaji wa huduma.
Akizungumza alipozindua kituo cha mizigo katika makao makuu ya shirika la reli jijini Nairobi, rais amesema ni jukumu la serikali kusikiliza matatizo yanayowakumba wananchi na kuyatatua na wala sio kusababisha matatizo zaidi.
Rais amesema kituo hicho kipya kinachofahamika kama Bomaline kitawapiga jeki wafanyibiashara haswaa wale wadogo wadogo ambao walikuwa wanalazimika kulipia ada za kusafirisha mizigo yao ambayo pia ilikuwa inachukua muda mrefu kufika jijini.