Rais Kenyatta atia saini mswada wa ugavi wa mapato

0

Hatimaye serikali za kaunti sasa zitapata mgao wa fedha waliotengewa katika mwaka wa kifedha wa 2020/2021.

Hii ni baada ya Rais Uhuru Kenyatta kutia saini mswada wa ugavi wa mapato uliopitishwa na bunge baada ya miezi kadhaa ya malumbano.

Serikali za kaunti sasa zitagawana shilingi billion 369.87 baada ya Rais kuongeza mgao huo kutoka shilingi billion 316.5 na kumaliza mgogoro kuhusu mswada huo.

Htaua hii ni afueni haswa kwa wafanayikazi wa kaunti ambao hawajapokea mishahara yao kwa zaidi ya miezi tatu.

Serikali za kaunti zilisitisha shughuli zake kwa muda kulalamikia hatua ya maseneta kukosa kupitisha mswada huo baada ya vikao kumi.

Rais Kenyatta ametia saini mswada huo katika ikulu ya Rais kwenye hafla ambayo imehudhuriwa na spika wa bunge la kitaifa Justin Muturi, waziri wa Fedha Ukur Yattani, kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa Amos Kimunya, mwenzake wa seneti Samuel Phoghisio miongoni mwa wengine.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here