Rais Kenyatta atakiwa kuwapa wakenya ‘uhuru’ (Audio)

0

Rais Uhuru Kenyatta ametakiwa kuondoa baadhi ya masharti yaliyowekwa kuzuia maambukizi ya virusi vya corona ile wakenya waendelee na shughuli zao za kawaida.

Mwanaharakati wa kutetea haki za kijamii Fredrick Ogweno anasema wengi wa wakenya wanaumia kutokana na baadhi ya masharti hayo ikiwemo amri ya kutotoka nje kati ya saa tatu na saa kumi asubuhi.

Rais Kenyatta anatazamiwa kulihutubia tena taifa kabla ya tarehe 26 mwezi huu kuelezea mikakati ambayo serikali imeweka kukabiliana na maambukizi hayo na iwapo ataondoa baadhi ya masharti yaliyowekwa.

Mojawapo ni amri ya kutotoka nje ambayo baadhi ya wakenya wanasema imeathiri sana biashara zao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here