Rais Kenyatta apendekeza Ann Nderitu kuteuliwa msajili wa vyama vya kisiasa

0

Rais Uhuru Kenyatta amependekeza kaimu msajili wa vyama vya kisiasa Ann Nderitu kuteuliwa rasmi kwenye wadhfa huo.

Katika taarifa kwa bunge la kitaifa, Rais amependekeza pia Ali Abullahi Surro, Florence Taabu na Wilson Muhochi kuteuliwa kama manaibu msajili.

Nderitu na wenzake watahojiwa na kamati maalum aya bunge la kitaifa kuhusu haki na masuala ya kisheria kabla yao kuteuliwa rasmi kuanza kuhudumu.

Kamati hiyo ina majuma matatu kufanya mahoajino na kuwasilisha ripoti ya ufaafu wa wanne hao bungeni kuidhinishwa au kukataliwa.

Nderitu amekuwa akishikilia wadhfa huo tangia Agosti mwaka 2018 wakati Lucy Ndungu aliondoka.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here