Rais Uhuru Kenyatta anaongoza mkutano wa baraza la Mawaziri katika Ikulu ya rais jijini Nairobi.
Mkutano huo unafanyika baada ya rais kuwatuma mawaziri katika likizo fupi.
Ni mkutano unaojiri wakati ambapo baadhi ya mawaziri wanashutumiwa kwa kujihusisha na siasa hali ambayo imedhihirisha mgawanyiko ulioko serikalini.