Rais Uhuru Kenyatta ameagiza bodi ya kitaifa ya nafaka na mazao NCPB kuwalipa wakulima waliowasislisha mahindi kwao kufikia Ijumaa wiki hii.
Katika taarifa, Rais Kenyatta pia ameagiza bodi hiyo kununua gunia ya mahindi kutoka kwa wakulima kwa zaidi ya shilling elfu 2500.
Rais Kenyatta pia ameagiza bodi hiyo kupunguza gharama ya kukausha mahindi kwa asilimia hamsini ili kupunguza gharama ya uzalishaji kwa wakulima.
Rais amesema serikali imeweka mipango ya kuwapa wakulima mashine za kukausha mahindi yao kufikia msimu ujao wa mavuno.