Raila Odinga akemea ukatili dhidi ya raia Nigeria

0

Mjumbe maalum wa miundo mbinu katika muungano wa Afrika (AU) Raila Odinga amekemea ukatili wa Polisi dhidi ya raia katika taifa la Nigeria.

Odinga katika taarifa amesema ukatili dhidi ya raia kufuatia maandamano ya wiki mbili kupinga uhalifu wa Polisi haufai na ni lazima suluhu la haraka lipatikane.

Kiongozi huyo wa upinzani aidha ametaka haki za kibinadamu kuheshimiwa huku akituma risala zake kwa waliofiwa kwenye patashika hiyo.

Shirika la Amnesty International linasema limepokea ripoti za maafisa wa Polisi kuwapiga risasi na kuwaua raia waliokuwa wanaandamana kupinga mauji hayo yanayodaiwa kutekelezwa na kitengo maalum cha Polisi wa kukabiliana na uhalifu SARS.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here