Raila na Ruto wagombana kuhusu IEBC

0

Naibu rais William Ruto ameitetea tume ya uchaguzi na mipaka IEBC kuhusu gharama inayofaa kutumia katika maandalizi ya kura ya maamuzi.

Akizungumza katika eneo la Kangema kaunti ya Murang’a, Ruto amemsuta kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga kwa kuingilia utendakazi wa IEBC akimtaka akome kuishurutisha tume hiyo inayoongozwa na Wafula Chebukati.

Ruto aidha ametaka kuwepo msimamo wa pamoja kuhusu ripoti ya BBI ili kuepuka kuwagawanya Wakenya kupitia mchakato huo wa kurekebisha katiba.

Wakati uo huo

Chama cha ODM kinasisitiza kwamba gharama inayohitajika kuandaa kura ya maamuzi haifai kuzidi Sh2b kinyume na msimamo wa IEBC kwamba ni Sh14b zinazohitajika.

ODM kupitia katibu wake mkuu Edwin Sifuna kinashikilia kuwa tume hiyo inapanga kutumia fursa hiyo ya kura ya maamuzi kuiba pesa za mlipa ushuru.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here