Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga anazuru kaunti ya Taita Taveta katika ziara ya siku mbili.
Odinga ameratibiwa kufanya mikutano na viongozi mbalimbali akiwemo gavana wa kaunti hiyo Granton Samboja.
Ziara ya waziri huyo mkuu wa zamani katika kaunti hiyo ya Pwani inajiri baada yake kukutana na viongozi wa mashinani katika kaunti ya Kakamega akiwemo gavana Wycliffe Oparanya.