Inspekta mkuu wa polisi Hillary Mutyambai ametetea idara hiyo kuhusina na shtuma kuwa wanaegemea upande mmoja katika kutekeleza sheria za kudhibiti mikusanyiko.
Katika taarifa kupitia kwa ukurasa wa Twitter, Mutyambai amesema wamekuwa wakiruhusu mikutano kutoka kwa baadhi ya makundi ambayo hayajakuwa na vurugu na kuzuia mikutano ya wanasiasa ambao mikutano yao imekuwa ikikumbwa na vurugu.
Mutyambai amesema kibali cha kuandaa mikutano kinategegemea na iwapo kuna athari ya kukumbwa kwa vurugu au la.
Anasema hawatasita kuendelea kufutilia mbali mikutano ambayo kuna uwezekano wa kuzuka kwa ghasia.
Haya yanajiri baada ya viongozi wa kundi la Tangatanga kulalama kuwa maafisa wa polisi wanatumiwa kuwanyima uhuru wa kuabudu na kutangamana huku wenzao kutoka vuguvugu la Kieleweke wakiruhusiwa kuandaa mikutano.