Polisi wamepewa maagizo ya kuanza rasmi kutekeleza kikamilifu kafyuu ya kutotoka nje kati ya saa nne usiku na saa kumi asubuhi bila mapendeleo.
Inspekta Jenerali wa Polisi Hillary Mutyambai amewataka Wakenya kushirikiana na vitengo vya usalama kuhakikisha kuwa maagizo hayo yamefuatwa.
Mutyambai amesema maeneo ya burudani yakayoendelea kufanya kazi baada ya saa tatu usiku yatafungwa huku magari ya uchukuzi ya umma yakipokonywa leseni zao,
Inspekta wa Polisi amesema Polisi watashirikiana kwa karibu na maafisa wa kaunti mbalimbali kuhakikisha kuwa mwongozo salama uliotolewa na wizara ya afya kuzuia msambao wa virusi hivyo unafuatwa.
Kimsingi, Mutyambai anamtaka kila mtu kuvalia barakoa na kuepuka mikusanyiko sawa na kusafiri pasipo kuwa na sababu.