Chris Obure, mmoja wa washukiwa kwenye mauaji ya Kevin Omwenga, Kilimani, Nairobi amepata pigo baada ya mahakama kutupa nje ombi lake la kutaka kufanywa kuwa shahidi badala ya kuwa mshukiwa kwenye mauji hayo.
Jaji Mumbi Ngugi akitoa uamuzi kwenye kesi hiyo ameamuru kuwa ombi la mshukiwa huyo halina misingi na kwamba mahakama haina ruhusa ya kuuamulia upate wa mashtaka kuhusu ni nani anafaa kuwa mshukiwa au shahidi.
Mahakama hiyo aidha imesema uamuzi kuhusu hilo utatolewa wakati wa kuendelea kwa kesi hiyo kwa kuzingatia ushahidi utakaowasilishwa.
Obure alikuwa amekataa kula kiapo kwenye kesi hiyo na badala yake kutaka abadilishwe na kuwa shahidi kwenye mauaji hayo yaliyotokea Agosti 21.