Mahakama Kuu imekataa kutupilia mbali maagizo ya kutaka Inspekta jenerali Douglas Kanja na mkuu wa DCI Mohamed Amin kuhudhuria vikao vya mahakama kutoa maelezo kuhusu kutekwa nyara na kutoweka kwa wanaume watatu huko Mlolongo mwaka jana.
Jaji Chacha Mwita amesema agizo hilo alilolitoa Januari mwaka huu lilikuwa na nia ya kudumisha katiba , kutekeleza Sheria na kulinda mfumo wa Haki.
“Kulinda maisha ya wanaume watatu waliotoweka kunasalia kuwa kipaumbele kwa mahakama hii. Haitakuwa kwa manufaa ya umma kuruhusu maombi ya IG na mkuu wa DCI,” amesema Mwita.
Kanja na Amin walitaka amri zitolewe Januari 8 na kutekelezwa Januari 13 kuwekwa kando wakidokeza hawakuarifiwa kirasmi kuhusu maagizo hayo ya mahakama.
Hata hivyo Jaji Mwiita amesema kuwa ameshawishika kuwa wawili hao walipokea hati za kesi hio kupitia anwani yao ya barua pepe.
“Kwa hiyo nimeshawishika kuwa walihudumiwa maombi na maagizo yaliyotolewa,” alisema.
Wanaharakati wakiongozwa na chama cha mawakili LSK walielekea mahakamani.
Ombi lao limejikita kwenye sheria ya Harbeus Corpus inayosema kuwa walio mikononi mwa polisi kufikishwa kortini chini ya masaa 24.