PAPA WA ROMA AFURAHI KUKUTANA NA PAPA FRANCIS.

0
wetangula meets pope francis
wetangula meets pope francis

Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetangula amekutana na Kiongozi wa kanisa Katoliki Papa Francis.

Picha za wawili hao zilizosambaa mitandaoni zimeonyesha wawili hao wakisalimiana katika makao rasmi ya Papa Francis inayotambulika kama “Apostolic Palace.”

Wetangula anaetambulika kwa jina la Utani “Papa Wa Roma” hajatoa maelezo kuhusu iwapo aliandaa majadiliano na Papa Francis.

“Nimefurahi sana kukutana na Mkuu wa Kanisa Katoliki,” ameandika Wetangula katika mitandao ya Kijamii.

“Papa Francis ni mfano wa Kiongozi Mtumishi wa kweli, ambae uongozi wake unaleta matumiani usawa na fursa kwa wasiobahatika,” ameongeza Wetangula.

Uongozi wa Papa Francis, Wetangula amebainisha, umejikita katika huruma, upendo, na ujasiri.

Wetangula yuko katika taifa la VATICAN kwa majukumu ya kikazi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here