Outtara ashinda uchaguzi wa muhula wa tatu Ivory Coast

0

Rais Alassane Outtara ameshinda muhula wa tatu wa Uchaguzi wa Urais nchini Ivory Coast, katika zoezi ambalo lilikumbwa maandamano, ghasia na upinzani kususia.

Tume ya uchaguzi nchini humo imemtangaza Outtara kuwa mshindi kwa kupata asilimia 94 ya kura zote zilizopigwa.

Ni asilimia 53 pekee ya wapiga kura nchini humo walishiriki zoezi hilo.

Maandamanao yalianza wakati Outtare alitangaza kuwania Urais kwa muhula wa tatu, upinzani ukimshtumu kwa kuhujumu demokrasia baada yake kubadilisha katba kumrushuu kuendelea kusalia uongozini.

Macho yote sasa ni kwa baraza la katiba nchini humo ambalo linatazamiwa kufanya uamuzi baada ya kuskiza lalama kutoa kwa pande husika ambazo hazijaridhika na uchaguzi huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here