Oscar Sudi kuendelea kulala kizimbani

0

Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi ataendelea kuzuiliwa kwa siku mbili zaidi akisubiri mahakama kutoa uamuzi kuhusu ombi lake la kuachiliwa kwa dhamana.

Sudi amefikishwa katika mahakama ya Nakuru Jumatatu ambapo upande wa mashtaka umeiomba mahakama kuruhusu mwanasiasa huyo kuzuiliwa kwa siku kumi na nne zaidi kuruhusu kukamilika kwa uchunguzi.

Miongoni mwa mashtaka dhidi ya mbunge huyo ni pamoja na kutoa matamshi ya uchochezi, kukataa kukamatwa, kumdhulumu afisa wa polisi na kumiliki silaha kinyume cha sheria.

Sudi alikamatwa jana Jumapili baada ya kujiwasilisha kwa kituo cha polisi cha Langas, mjini Eldoret.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here