Oscar Sudi asema kuna njama ya kufufua kesi za ICC kumzuia Ruto

0

Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi sasa anadai kuwa kuna njama ya kufufua kesi za ICC katika juhudi za kumzuia naibu rais William Ruto kuwania urais kwenye uchaguzi mkuu wa 2022.

Sudi kupitia taarifa amedai kuwa hatua ya kujisalimisha kwa wakili Paul Gicheru ambaye amekuwa akisakwa na mahakama hiyo huenda ni katika juhudi za kuhakikisha kuwa mipango hiyo imefaulu.

Hata hivyo mbunge huyo mwendani wa Ruto amesema njama hizo hazitafaulu akidai kuwa itakuwa vigumu kufufua kesi hizo pasipo kumuhusisha rais Uhuru Kenyatta.

Wakili Gicheru anatazamiwa kufunguliwa mashtaka ya kutumia njia za kifisadi kuhitilafiana na mashahidi kwenye kesi ya vurugu za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here