Orodha ya Wakenya wanaofadhili ugaidi yatolewa

0

Waziri wa usalama wa ndani Dkt. Fred Matiang’i ametoa orodha ya Wakenya tisa wanaotuhumiwa kufadhili shughuli za kigaidi hapa nchini.

Akaunti za washukiwa hao wanaodaiwa kufadhili shughuli za kundi la kigaidi la Alsha baab wakiwa humu nchini zitafungwa huku mali zao zikitwaliwa kwa mujibu wa agizo la waziri Matiang’i.

Wakenya hao wanajumuisha Halima Ali, Waleed Zein, Sheikh Boru, Mohammed Ali, Nuseiba Haji, Abdimajit Hassan, Mohammed Ali Abdi, Muktar Ali na Mire Elmi.

Waziri Matiangi katika taarifa amesema asasi za usalama zitaendelea kujitahidi vilivyo kuzima shughuli zozote za kigaidi hapa nchini ili kuwahakikisha Wakenya usalama wao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here