Optiven yamjengea mama nyumba Machakos

0

Wakfu wa Optiven umepeana nyumba dhabiti kwa mama wa watoto watano katika kijiji cha Ivovoani, katika jimbo la Machakos. Haya yanajiri baada ya wakfu huo kuingilia kati baada ya msaidizi kutoa habari hizo za hali duni ya maisha walimo kuwa wakiishi jamii hiii.

Aliyenufaika ni na nyumba hiyo ni Mama Nduku ambaye pamoja na kuishi katika hali duni, anaugua kifafa na amehitajika kuwahangaikia watoto wake tano baada ya mume wake kumtelekeza. Lakini mazingira yalibadilika wakati majirani, wadau na washiriki wa kanisa walijiunga katika nyimbo na mbwembwe kwa niaba ya Mama Nduku.

Akizungumza katika hafla ile, George Wachiuri, Mwenyekiti wa Wakfu wa Optiven, waliwataka wote kuchukua wakati wa sikukuu kama nafasi nzuri ya kuwasaidia wale wasio jiweza. Wachiuri aliongeza, “sikukuu hii sote tunaweza kuwa Baraka kwa watu wazima walio sahaulika na wananchi ndio washirikishi wa wakfu wa Optiven kule wanakoishi”.

Aliongeza kuwa, mfano wa ujenzi uliotumika kuijenga ile nyumba uli zingatia nishati mbadala na inayo dumu.

Hii ni sehemu ya kampeni iliyozinduliwa na Optiven kwa jina #GoGreenNaOptiven mnamo mwezi Novemba mwaka huu.

Wakfu wa Optiven, una dhaminiwa na kitengo cha uuzaji mashamba chini ya kikundi cha makampuni ya Optiven Group na hutoa asili mia tano ya mapato yake kutokana na uuzajia mashamba. Wakfu huo umejenga nyumba hapo awali kuwa nufaisha wasio jiweza.

Katika tukio la hivi karibuni, Wachiuri anasema, ‘wakfu wa Optiven umetoa nyumba dhabiti, na kuijaza vitu vya nyumbani pamoja na kutoa msaada wa mafunzo kwa mtoto wa Mama Nduku aliye mwanafunzi katika chuo kikuu’.

Nyumba hiyo ili pokezwa rasmi na Askofu wa Kanisa la Destiny Life akiwa na Bwana Wachiuri. Sherehe hivyo ili hudhuriwa na wasimamizi wa wakfu huo, wawakilishi wa makanisa, na serikali ya majimbo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here